Wakati ambapo dunia ikiweka jitihada zote kuisaka ndege ya shirika la Malaysia aina ya Boing 777 iliyopotea ikiwa na watu 239 wakati ikielekea Beijing, mhubiri maarufu wa Nigeria T.B Joshua ametoa utabiri kuwa ndege hiyo imezama baharini!
Jumapili iliyopita, T.B Joshua ameeleza kanisani kwake (SCOAN) kuwa ndege hiyo ilianguka na imezama ndani kabisa kwenye tope za bahari na kwamba hivi karibuni vipande vya ndege hiyo vitaanza kuonekana vikielea.
“Ndege hiyo iko ndani kabisa ya bahari. Baadhi ya vipande vitaanza kuonekana vikielea baharini muda wowote kuanzia sasa." Alisema T.B Joshua.
“Roho zao zipumzike kwa Amani. Tunaomba bwana azipe familia zao na wapendwa wao nguvu/uimara kushinda upotevu huu. Maombi yetu na upendo viko nao, nchi ya Malaysia na nchi nyingine ambazo zilikuwa na abiria katika ndege hiyo.” Alisema T.B Joshua kwa mujibu wa mtandao wa Nigeria wa Informationnng.
Hayo ni mambo ya imani!
Wakati dunia ikiwa bado haijafahamu ilipo ndege hiyo, wizara ya mambo ya nje ya China imeitaka Malaysia kuharakisha juhudi zake za kuitafuta ndege hiyo iliyokuwa na abiria 154 raia wa China kati ya abiria 239 waliokuwa katika ndege hiyo.
Ndege hiyo ilipotea mwishoni mwa juma na kumekuwa na mashaka kwamba huenda ni bomu au utekaji nyara unaweza kuwa uliiangusha ndege hiyo

No comments:
Post a Comment