TAARIFA YA PINGAMIZI LA MGOMBEA WA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE .
FABIAN LEONARD SKAUKI – MGOMBEA CHAMA CHA WANANCHI –CUF
DHIDI YA
MATHAYO MANG’UNDA TORONGEY – MGOMBEA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO -CHADEMA
13.03.2014
Mimi FABIAN L. SKAUKI,
mgombea ubunge wa uchaguzi mdogo jimbo la CHALINZE kwa Ticket ya THE
CIVIC UNITED FRONT (CUF) ninamwekea Pingamizi mgombea wa chama cha
demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwamba amepoteza sifa za kuwa mgombea kwa sababu zifuatazo.
1. Ndugu
MATHAYO. M. TORONGEY amejaza Taarifa za uongo kwenye Fomu yake kwamba
kazi anayoifanya ni BIASHARA. Sio kweli, kwa sababu hajaweka vielelezo
vya yeye kufanya hiyo kazi. Hajulikani anafanya kazi gani.
2. Ndugu MATHAYO .M. TORONGEY amejaza katika
fomu kwamba anajua kusoma na kuandika Kiswahili na kiingereza. Taarifa
hizi ni za uongo, mgombea huyu hajui kusoma wala kuandika Kiswahili wala
kiingereza, na kwamba amedanganya na amepoteza sifa za kuwa mgombea.
3. Ndugu MATHAYO .M.TORONGEY amedanganya
kwa kughushi/kufoji sahihi za wadhamini,ambao amewaorodhesha kwenye
fomu ya kuomba kuthibitishwa kuwa mgombea. Ambapo katika fomu hizo
wadhamini wote sahihi zao zimefojiwa na hazifanani na zile zilizokuwepo
kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba sahihi zote hizi
zimesainiwa na mtu mmoja ambaye sio muhusika. Hivyo anapoteza sifa ya
kuendelea kuwa mgombea.
4. Ndugu
MATHAYO.M.TORONGEY ameshindwa kutimiza mahitaji ya kisheria ya kuwa na
wadhamini wasiopungua 25, badala yake amedhaminiwa na wadhamini 28 ambao
kati yao wadhamini 7 sio wapiga kura halali wa jimbo la CHALINZE, na
kwamba Taarifa zao na namba zilizojazwa hazifanani.
Hivyo anabakiwa na wadhamini halali 21 ambao kisheria hawatoshi kutimiza matakwa ya kisheria.
No comments:
Post a Comment