Saturday, March 1, 2014

Dr.MAGUFULIAKAGUA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI JIJINI DAR ES SAALAM

Dr.John Magufuli kwa mara nyingine amefanya ukaguzi wa maendeleo ya mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (BRT) Jijini Dar es Salaam akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Katibu Mkuu- Ujenzi, Katibu Mkuu -TAMISEMI, Kamati ya Ulinzi na Usalaam ya Mkoa wa Dsm, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara-TANROADS,Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Haraka -DART, Meneja wa Ujenzi wa Mradi pamoja na wadau mbalimabli wa mradi wakiwemo wananchi.
Dr.Magufuli amehoji kiasi kikubwa cha mzigo kupitia barabarani badala ya reli, ambapo asilimia 98.7 ya mizigo inayosafirishwa mikoani inapita barabarani hasa kutoka DSM kwenda Tunduma sehemu inayofikika kwa reli.
Ili kupunguza msongamano, amesema miradi saba (7) iliyopo jijini Dsm ipo mbioni kusainiwa wakatai wowote, hata hivyo amesisitiza wananchi wa kada zote kufuata sheria zilizowekwa ikiwa ni pamoja na kupisha hifadhi za barabara, sheria za barabara n.k.
Aidha, Dr.Magufuli amegusia na kusisitiza kuanza kwa ujenzi wa barabara ya kiwango cha EXPRESSWAY inayotoka Dar - es Salaam hadi Chalinze yenye urefu wa kilomita 100, barabara hii itakuwa ya njia sita hadi nane kila upande. Makampuni yapatayo kumi na tisa yameonyesha nia ya kuwekeza kwa kuingia ubia na Serikali ya Tanzania kupitia utaratibu wa Public Private Partnership (PPP). Kwa kuzingatia kiwango cha EXPRESSWAY mradi huo utahitaji eneo kubwa la ujenzi (Construction Corridor) . Dr.Magufuli amewakumbusha wananchi waliovamia hifadhi ya barabara (Road Reserve) kupisha mara moja ili kuepuka usumbufu kipindi mradi utakapoanza, pia amewashauri wananchi wasipotoshwe na baadhi ya watu kuhusu hifadhi ya barabara ya Morogoro kwa kuwa upana wa barabara hii unajulikana kuwa ni tofauti na barabara zingine nchini, yeyote atayekaidi kwa kutumia kesi batili atafikishwa mahakamini.
Picha za matukio ya msafara wa waziri wa Ujenzi Dr.Magufuli;







Ndani ya Basi liendalo Haraka




Wakala wa Usafiri wa Haraka -DART


Kazini

Akipata Maelezo ya Mradi


Akipata Maelezo ya Mradi kutoka kwa Meneja wa Mradi-TNROADS

No comments:

Post a Comment