Friday, March 7, 2014

BOSCO NTAGANDA APELEKWA ICC


     Bosco ntaga
 Mtuhumiwa wa makosa ya kivita wa Jamuhuri ya Kidemokria ya Kongo katika mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC, Bosco Ntaganda yupo njiani kuelekea katika sero ya Mahakama hiyo mjini The Hague.
Generali Ntaganda ambaye alikuwa mhimili wa mgogoro wa Kaskazini mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, alijisalimisha katika ubalozi wa marekani mjini Kigali nchini Rwanda siku ya jumatatu.
Bosco Ntaganda anakabiliwa na mashtaka kumi ya makosa ya kivita na uhalifu dhidi ya binadamu ambayo amekuwa akiyakana.
Tarehe kamili ya kusikilizwa kwa kesi yake inatarajiwa kujulikana hivi karibuni.
Bosco Ntaganda ni mtuhumiwa wa kwanza kujisalimisha mwenyewe katika mahakama hiyo ya ICC.
Kwa upande wake Mwendesha mashtaka Mkuu wa mahakama hiyo Fatou Bensouda amesema kujisalimisha kwa Ntaganda limekuwa ni jambo zuri.
"Hii ni siku njema kwa waathirika wa vita nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na katika utoaji haki duniani."Bi Fatou Bensouda aliambia BBC katika kipindi cha Focus on Afrika.
"Leo wale wote walioathirika na mkono wa Bosco Ntaganda sasa wataangalia sheria ikichukua mkono wake" Amesema Bi Bensouda.
Akijulikana kwa jina la "The Terminator" Ntaganda alipigana na makundi kadhaa ya waasi na pia aliwahi kuwa askari wa Jeshi la Serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Katika siku za hivi karibuni inaaminika alikuwa mmoja wa viongozi wa kundi la waasi wa M23 ambalo limekuwa likipigana na majeshi ya serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

No comments:

Post a Comment