Friday, March 14, 2014

BAJAJI, BODABODA MARUFUKU KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM



Wakihojiwa na TBC 1,Kamanda wa polisi bwana Sulemani Kova,Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam bwana Saidi Mecki Sadiki ,pamoja na Afisa Mfawidhi kanda ya mashariki,Conrad Shio wa Mamlaka ya Usafiri wa Majini na Nchi kavu (SUMATRA) wameweza kuelezea jinsi mchakato huu utakavyokuwa jijini Dar es Salaam.
Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Kanda ya Mashariki Bw. Conrad Shio akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu sheria inayosimamia usafiri wa Bajaji na Bodaboda nchini.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamishna (CP) Suleiman Kova akitoa ufafanuzi ameeleza kwa waandishi wa habari kuhusu wakazi wa jiji la Dar es salaam hususan madereva wa bodaboda na Bajaji kufuata sheria za barabarani na kajenga tabia ya kufanya tathmini ya safari zao iwapo wanakidhi vigezo vya usalama barabarani ili kuepusha madhara.
Wote waliweza kutoa sababu mbalimbali ya kwanini wameamua kushirikiana katika kuhakikisha vyombo hivi vya usafiri haviingii sehemu za mijini.
Vyombo hivi vya usafiri yaani bajaji,bodaboda na maguta ( baiskeli zenye matairi matatu) vitakatazwa kuingia sehemu zote za CBD (mijini).
Wakitolea mifano wa sehemu hizo ni,ukitokea Bunju hadi kuja Tegeta,mwisho wa vyombo hivyo utakuwa ni Mwenge
Pia ukitokea Mbezi ya Msuguli mwisho itakuwa Kimara kwahiyo ukija Ubungo utazuiliwa.
Kwahiyo maeneo yoote ya mijini Posta ikiwemo,vyombo hivi havitaruhusiwa kuingia

SABABU ZA KUZUIWA KUINGIA.
Viongozi hawa watatu waliweza kutoa sababu mbalimbali za kwanini vyombo hivi vimekatazwa kuingia sehemu za mijini.
Sababu hizo ni kama zifuatazo
 1.Kuzuia matukio ya ualifu yanayofanyika kwakutumia sana bodaboda.Yaani bodaboda zinatumika sana kwenye matukio ya uhalifu kama wizi na ujambazi.
2. Kuzuia msongamano wa vyombo vya usafiri jijini.
3. Kupunguza ajali zinazosababishwa haswahaswa na vyombo hivi mfano bodaboda.kamanda Kova alitolea mfano kuwa unakuta kijana wa bodaboda yupo mataa lakini hata kama taa hazijamruhusu yeye anapita na kuacha magari kubakia kwenye mataa. Hapa aliuliza kwani waliosimama sio watu???? Kwahiyo alisema vyombo hivi madereva wake wengi hawafati sheria za barabarani
HITIMISHO.
Walisisitiza kuwa vyombo hivyo vimeruhusiwa kwa shughuli za biashara pembezoni mwa jiji la Dar es Salaam.
Pia kwa wale watu wanaotumia kama usafiri wao binafsi yaani sio kibiashara wanaruhusiwa kuingia navyo mijini hususani pikipiki kwa sharti la kuwa pekee yaani bila kumpakiza mtu nyuma.

Kamanda Kova aliongeza na kusema,kama mtu akitoka pembezoni mwa mji mfano Bunju au Tegeta basi akifika Mwenge ambapo ndio mwisho wa bodaboda za biashara, atatakiwa achukue usafiri wa umma na kuendelea na safari zake.
Kamanda Kova alisema kama sheria inatakiwa itende haki kotekote maana kuna watu wanaweza kudanganya kuwa pikipiki anayoiendesha siyo ya biashara kwahiyo mtu aliyembeba ni rafiki au mpenzi wake na ikachukuliwa kawaida lakini itaonekanaje kwa wale wafanya biashara wanaopakiza nao watu kama hawa??? Kwahiyo sharti ni uwe mwenyewe kwenye pikipiki yako.
Naye Afisa Mfawidhi wa SUMATRA Kanda ya Mashariki Bw. Conrad Shio ameeleza kuwa sheria ya usafirishaji kusimamia Bajaji na Bodaboda iko wazi na kuongeza kuwa serikali ina wajibu wake na pia waendesha pikipiki na Bajaji wanawajibu wao wa kuzingatia kanuni taratibu na kanuni zilizowekwa.
“Sisi kama SUMATRA tunaendelea kufanya kila tuwezalo kukabiliana na vitendo vyote vya uvunjivu wa sheria za barabarani”






No comments:

Post a Comment