Na Ibrahim Yamola na Beatrice Moses, Mwananchi
Dar es Salaam.
Serikali
imesitisha ajira 70 za konstebo na koplo wa Uhamiaji baada ya kuzuka
kwa tuhuma za upendeleo uliokithiri wakati wa usaili.
Agizo
hilo la Serikali lilitolewa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya
Ndani, Mbarak Abdulwakil ambaye ametengua kauli yake ikiwa ni wiki mbili
tu tangu alipozitangaza nafasi hizo.
Mara
baada ya ajira hizo kutangazwa, wadau mbalimbali walianza kulalamika
kwa madai kwamba nafasi hizo zimetolewa kwa upendeleo kwa ndugu na
marafiki wa watumishi wa Idara ya Uhamiaji.
Taarifa
kwa umma iliyotolewa jana na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Isack
Nantanga ilisema Abdulwakil amesitisha ajira hizo baada ya kuzagaa kwa
tuhuma za upendeleo kwa ndugu na jamaa wa watumishi wa idara hiyo.
“Kutokana
na kusitishwa kwa zoezi hili, waombaji wote walioitwa na kutakiwa
kuripoti makao makuu ya Idara ya Uhamiaji Agosti 5 mwaka huu sasa
watatakiwa kusubiri hadi hapo watakapotangaziwa tena.”
Ilisema Abdulwakil ameunda kamati ndogo kuchunguza tuhuma hizo na ikikamilika ndipo uamuzi utakapofanyika.
Hatua
hiyo imechukuliwa kutokana na tuhuma zilizotolewa na baadhi ya vyombo
vya habari na mitandao ya kijamii kwamba kulikuwapo na upendeleo wakati
wa usaili.
Julai 13 mwaka
huu, Idara ya Uhamiaji ilifanya usaili wa kujaza nafasi 70 za mkaguzi
msaidizi wa Uhamiaji uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waliopita ni 6,115 ambao walichujwa na kufika 1,681 walioingia katika kinyang’anyiro cha kusaka watumishi 70.
Utata ulivyo
Baadhi
ya waliotakiwa kuripoti Agosti 5 mwaka huu wanaodaiwa kuwa ni watoto au
ndugu wa wafanyakazi wa idara hiyo ambao majina yao yalisambaa katika
vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ni: Abdulhaq Amin Mandemla –
Mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Amin Mandemla, Alphonce Kishe – Mtoto wa Ofisa
Uhamiaji, Aleluya Kishe na Asha Burhani Idd – ndugu wa Ofisa Uhamiaji na
Tatu Burhani Idd.
Wengine ni
Beatrice Temba – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Joseph Kasike, Geofrey
Justine Mhagama – ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Rose Mhagama, Iginga Daniel
Mgendi – Mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Daniel Mgendi na Issack Michael
Makwinya – mtoto wa aliyekuwa Ofisa Uhamiaji, Makwinya.
John
Alfred Mungulu – mtoto wa Ofisa, Uhamiaji Alfred Mungulu, Joseph A.
Milambo - mtoto wa Karani wa Uhamiaji, Milambo, Michael J. Choma – mtoto
wa Ofisa Uhamiaji, John Choma, Shimba H Zakayo – mtoto wa Ofisa
Uhamiaji, Zakayo Mchele na Upendo E. Mgonja - mtoto wa Ofisa Uhamiaji
Mgonja.
Wengine ni Vaileth A.
Kidesu – mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Adam Kidesu, Elizabeth Edward – ndugu
wa Ofisa Uhamiaji, Edward Martin, Ester Mahirane – ndugu wa Ofisa
Uhamiaji, Mahirane na Basil Lucian John – ndugu wa Ofisa Uhamiaji,
Dismas Lucian.
Frank E
Kajura- ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Kajura, Jacob P. Ulungi – ndugu wa
Ofisa Uhamiaji, Magnus Ulungi, Janeth John Milinga – ndugu wa aliyekuwa
Ofisa Uhamiaji, Milinga, Janeth R Lukuwi – ndugu wa Ofisa Uhamiaji Eliza
Lukuwi, Joseph N. Yondani – Mtoto wa Ofisa Uhamiaji, Mary Yondani.
Leila
Khatib Irovya - Mtoto wa Ofisa Uhamiaji Abbas Irovya, Lucian F. Mlula –
ndugu wa Ofisa Uhamiaji, Dismas Mlula, Neema Kasian Lukosi- ndugu wa
Ofisa Uhamiaji, Zubeda Abbas, Pendo D. Gambadu – ndugu wa Ofisa
Uhamiaji, Gambadu, Paschalia E. Mwenda – ndugu wa Martin Edward Mwenda.
Theresia
Ernest Kalunde – mtoto wa Ernest Kalunde, Veronica G Vitalis – mtoto wa
aliyekuwa Ofisa Uhamiaji Vitalis Mlay, Victor G. Mlay- mtoto wa
aliyekuwa Ofisa Uhamiaji, Vitalis Mlay na Catherine J. Mapunda- mtoto wa
Ofisa, Lucy Mapunda.
Uhamiaji wajitetea
Idara ya Uhamiaji imekiri kupokea malalamiko yaliyotolewa dhidi yake.
Kaimu Msemaji wa Idara ya Uhamiaji, Rosemary Mkandala alisema jana kuwa wamepokea tuhuma hizo na wanazifanyia kazi.
“Ninaomba
tu wale ambao walishiriki kwenye usaili huo na wana malalamiko
wayawasilishe rasmi ili tuweze kuyafanyia kazi. Suala linachunguzwa sasa
na matokeo yake yatabainisha kama kuna ukweli au la,” alisema
CHANZO: MWANACHI
No comments:
Post a Comment