Ni
mamia ya wakazi na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya walioamua kwenda
kumpokea Diamond Platnumz baada ya safari yake ya kutoka Marekani
ambayo imekua njema kwa Tanzania baada ya kurudi na tuzo.
Mapokezi yalianzia uwanja wa Julius Nyerere International Airpot
kisha msafara ukaelekea mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam
ukipitia Buguruni,Kariakoo na baadae kumalizia nyumbani kwake Sinza.
Wakati
akiwa kwenye gari ya wazi Diamond Platnumz muda wote alikua kaishikilia
tuzo yake aliyoipata Marekani kwenye tuzo za AFRIMMA ambapo kwa upande
wake ameibuka na ushindi wa tuzo ya Msanii bora wa Afrika Mashariki.
Ratiba ya Diamond kuingia Tanzania ilikua iwe jioni ya Jana July 29
lakini kutokana na sababu walizosema zilizokuwa nje ya uwezo wao safari
yao ikasogezwa mpaka leo July 30 na alifanikiwa kuingia saa 1 asubuhi.
Ingawa hali ya hewa ilikua imetawaliwa na manyunyu pamoja mvua ndogo
ndogo,Hizi ni baadhi ya picha za mashabiki waliojitokeza kumpokea
Diamond.
GREDIT MILLARD AYO
No comments:
Post a Comment