Wednesday, April 23, 2014

POLISI WAMNYIMA LEMA KIBALI CHA KUFANYIA MKUTANO JIMBONI KWAKE ARUSHA

Name:  TAARIFA YA KUSITISHA MIKUTANO YA HADHARA.jpg
Views: 0
Size:  480.6 KB 
Hii ni barua kutoka kwa OCD  wa wilaya ya Arusha kwenda kwenda kwa Lema. 
 


Tarehe 17/4/2014 Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema aliandika barua yenye kumbukumbu na (MB./OCD/ARMJN/17/2014) kwa OCD wa wilaya ya Arusha Giles Mroto, akitoa taarifa ya kufanya mikutano ya hadhara katika kata za Jimbo lake la Arusha Mjini. Barua yenye kumbukumbu tajwa hapo juu OCD Mroto aliijibu barua ya Mbuge Lema tarehe hiyo hiyo ya 17/4/2014 kwa barua yenye kumb. (AR/B.5/VOL.III/160) akiruhusu Mbunge Lema kufanya mikutano katika kata mbili tu ambazo ni Daraja mbili na Moshono.

Jambo la kusikitisha na kutia hasira kutokana na utendaji mbovu wa OCD wa Arusha Giles Mroto ni pale alipoandika barua nyingine yenye kumbukumbu no. (AR/B.5/VOL.III/162) ya kuzuia mikutano ya Mbunge Lema katika kata mbili kwa hoja dhaifu, zisizo na mashiko kama ifuatavyo:

  1. Tarehe ambayo Mbunge Lema ametoa taarifa ya kufanya mikutano, CCM wilaya ya Arusha wameomba kufanya mikutano ya hadhara, akirejea kwenye barua ya ccm iliyoandikwa tarehe 19/4/2014 yenye kumb. na. (CCM/AR/U.4/VOL.III/2014/72). Kwa mujibu wa barua ya OCD Mroto CCM katika barua yao wameomba kufanya mikutano Levolosi, Terat, Daraja Mbili na Moshono kuanzia Tarehe 20/4/2014 hadi 25/4/2014.
  2. Mikutano ya Lema imekataliwa kufanyika kutokana na tukio la mlipuko wa Bomu katika baa ya Arusha Night Park, hivyo kutokana na hali ya usalama kuwa imara.




No comments:

Post a Comment