Wednesday, September 9, 2015

DIAMOND ATAJWA ACHAGULIWA TENA KWENYE TUZO ZA KIMATAIFA



Msanii wa Bongo Flava Diamond Platnumz anazidi kuipeperusha bendera ya Tanzania, Tuzo nyingi sana zinazidi kutambua juhudi na kazi ya Diamond kwenye muziki wa Tanzania.


Good news kwako mtu wangu, mtu wetu Diamond Platnumz amepata nafasi nyingine kubwa ya kuiwakilisha Tanzania kwenye tuzo za kimataifa.



Tuzo za MTV Europe Awards maarufu kama MTV EMA kwa mwaka huu wa 2015 zimemtaja Diamond Platnumz kuwa miongoni mwa wasanii kutoka Africa wanaowania kipengele cha ‘Best African Act’, wasanii wengine waliobahatika kuingia kwenye kipengele hicho ni; Davido, AKA (South Africa) na Yemi Alade (Nigeria).



Yemi Alade ni msanii pekee wa kike kwenye kipengele hiki cha Best African Act.



Davido kutoka Nigeria


AKA kutoka South Africa.
MTV EMA 2015 inahitaji mtu wa tano kukamilisha orodha ya ‘Best African Act’ mtu wangu na kama wewe ni mdau mkubwa sana wa muziki mzuri basi MTV EMA 2015 inakupa wewe nguvu na kibali cha kumchagua mtu wa 5 unaehisi atafaa kuchuana na Diamond Platnumza na wengine kwenye kipengele hiki..




kwenye wale watano waliopendekezwa wapo; Wizkid, KO (South Africa), Stone Bwoy (Nigeria), Cassper na DJ Arafat.




Kumpata mmoja kati ya watano hapo juu, utaratibu wa kuwapigia kura upo hivi… unaandika #MTVEMA ikifuatiwa na hashtag (#Nominate) na jina la msanii na kisha unatweet mara nyingi uwezavyo kwenye Twitter ili kumpata yule unayeona anastahili kufunga kipengele hiki.




Tuzo za MTV EMA Awards 2015 zinafanyika tarehe 25 October jijini Milan, Italy. Mwisho wa kupiga kura ni tarehe 14 September 2015.

Monday, June 8, 2015

MILLARD, DIAMOND, SHERIA NGOWI, DK. MENGI, ZITTO WALAMBA TUZO KATIKA KONGAMANO LA WANAVYUO DAR




Dkt. Kitila Mkumbo akipokea tuzo ya mwanasiasa anayependwa sana na mwenye mvuto kwa jamii ambayo tuzo ilienda kwa Zitto Kabwe.



Mlezi Dkt. David Rweikiza akitoa tuzo kwa mwanamitindo anayependwa ambayo tuzo ilienda kwa Sheria Ngowi, alipokelewa na mwakilishi wake.



Mkurungezi wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, akitoa tuzo kwa mtangazaji anayependwa ambayo tuzo ilienda kwa Millard, tuzo ilipokelewa na mwakilishi wake anayefahamika kwa jina la Askofu.
Mkurungezi wa AEG LTD, Iman Kajula akitoa tuzo kwa Diamond Platinumz kama msanii anayependwa, tuzo ilipokelewa na mwakilishi wake Nikki wa Pili.
Mkurungezi wa IPP Media, Dkt. Reginald Mengi akitoa shukrani kwa waandaaji wa tuzo hizo.
Washindi na wawakilishi wa tuzo mbalimbali zilizotolewa kwenye kongamano hilo.



Mwenyekiti wa Chama cha Wanafunzi wanaosoma Kitivo cha Masoko cha Chuo Kikuu UDSM (DUMA), Dkt. Ulimwengu akitoa historia fupi ya Tuzo za ACHIVERS AWARDS katika kongamano la wanafunzi wanaosoma Kitivo cha Masoko na Biashara lililofanyika Jumamosi iliyopita UDSM na kukutanisha wanataaluma wengi na wajasiriamali waliofanikiwa. Kongamano hili lilikutanisha vyuo mbalimbali ikiwemo UDSM, IFM, CBE, na TIA.


Mkurunezi wa IPP Media, Dk. Regnald Mengi akitoa hamasa ya wanafunzi kuweza kutumia fursa kuweza kutengeneza mawazo ya kibiashara katika kongamano la wanafunzi wanaosoma masomo ya Masoko na Biashara


Wanafunzi wakifuatilia kwa makini kongamano hilo la 'Marketing Forum'.


Washiriki wa kongamano wakionekana kushangilia baada ya Dk. Mengi kuwa anatarajia kuzindua kitabu chake kipya mwishoni mwa mwaka huu.
Mkurungezi na Mwanzilishi wa Mwanaharakati Mzalendo Media pia Mkurungezi Mtendaji wa Kajo Itech ambao walikuwa ni wadhamini rasmi wa kongamano hilo, Krantz Mwantepele akiongea na wanafunzi jinsi gani wanaweza kufungua fursa za baishara na kuweza kujiajiri kutumia mitandao ya kijamii.

(PICHA / HABARI: MWANAHARAKATI MZALENDO MEDIA)

JANUARY MAKAMBA ALIVYOTHIBITISHA KUGOMBEA URAIS TANZANIA 2015

 



June 07 2015 mmoja kati ya Viongozi ambao wameingia kwenye headlines za kutajwa kwamba na yeye anahitaji kusogelea njia ya kuingia Ikulu ya TZ kwenye Uchaguzi wa mwaka huu 2015 ni Naibu Waziri, January Makamba.

Tayari kathibitisha kwamba ana lengo hilo, kutoka Mlimani City Dar hapa nina nukuu ya baadhi ya sentensi zake wakati akitangaza nia hiyo.

“Nimeona nitumie siku ya leo kuwajulisha kwamba nimeamua kuomba nafasi ya Rais wa Tanzania… keshokutwa nitakwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya CCM ili niteuliwe kugombea mwaka huu.. Naelewa kiu ya Watanzania kupata aina mpya ya uongozi utakaotoa matumaini mapya yatakayozaa Tanzania mpya“>>>

“Siko mbele yenu leo kuwasimulia matatizo ya Watanzania.. niko mbele yenu kueleza tutakavyotatua matatizo ya nchi yetu. Nitaunda Serikali ya Mawaziri wasiozidi 18, haitakuwa na mtu hata mmoja anaetiliwa shaka kuhusu uadilifu wake wala uwezo wake“>>>

“Kwenye Serikali yetu tutataka kila mtu afuate Sheria za nchi hata ziwe ndogo kiasi gani.. Tutakabiliana na tatizo la ubadhilifu wa mali za umma kwa nguvu zetu zote“>>>

“Viongozi wengi wa siasa wameliita tatizo la ajira kuwa ni bomu lakini kulielezea tatizo la ajira sio kulitatua.. tukiwezesha 80% ya biashara ndogondogo hapa nchini zitakuwa zimepunguza kama sio kumaliza kabisa tatizo la ajira”>>>

“Tutaongozwa na dira ya elimu inayochochea vijana kujiajiri“>>>

“Ualimu ni wito, hatutaki ualimu uwe adhabu.. Tutazitatua changamoto za Walimu, hatutaingiza Siasa kwenye elimu“>>>– January Makamba.











CREDIT MILLARD AYO
 

PICHA ZA MAANDALIZI YA VIDEO MPYA YA ALLY KIBA SOUTH AFRIKA



Ali Kiba staa mwingine mkali wa muda mrefu kwenye Bongo Fleva… Hit ya Chekecha Cheketua ni moja ya ngoma ambazo mtaani wanaisubiri video yake kwa hamu sana.

Nakumbuka Abdu Kiba aliwahi kusema kwamba kazi ya video ya wimbo huo itafanywa Afrika Kusini… hizi ni dalili kwamba video mpya ya Ali Kiba itakuwa on air muda wowote japo katika post zake hajasema video anayoshoot ni ya wimbo gani.

PICHAZ ambazo Ali Kiba ameanza kuzishare mfululizo kwenye ukurasa wake @Facebook ni hizi.



Hii ilikuwa post ya kwanza aliyoweka Ali Kiba kabla ya kuanza kupost pichaz hizo.














 

Monday, June 1, 2015

AJALI YA LORI LA MAFUTA YAUWA NAIGERIA



Nigeria imeendelea kukumbwa na matukio ya vifo, baada ya tukio la kundi la Boko Haram kuvamia msikiti na kuuwa watu 16 jana, kuna taarifa nyingine ambayo si nzuri kutoka nchini humo.
Watu wasiopungua 70 wamefariki dunia Mashariki mwa Nigeria baada ya lori la kubeba mafuta kushika moto huku magari mengine 15 nayo yakishika moto.
Mashuhuda wa ajali hiyo iliyotokea jana wamesema dereva wa gari hilo alishindwa kudhibiti mwendo kazi wa gari hilo ndipo likakosa mwelekeo na kutoka barabarani na kuwagonga watu waliokuwa wakisubiri usafiri katika kituo kimoja cha mabasi.

KATIBU MKUU MPYA WIZARA YA MAMBO YA NJE BALOZI LIBERATA MULAMULA AKABIDIWA OFISI RASMI



Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akikabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi John Haule. Kabla ya uteuzi huo Balozi Mulamula alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mhe. Haule kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya. Makabidhiano hayo yalifanyika Wizarani leo tarehe 01 Juni, 2015.



Katibu Mkuu, Balozi Mulamula akiwa kwenye Mkutano na baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo mara baada ya kukabidhiwa rasmi Ofisi na Balozi Haule.


Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Nigel Msangi (wa kwanza kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga (wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango Bw. James Lugaganya na Balozi Haule wakimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani\

WAZIRI NYALANDU KUCHUKUA FOMU YA URAISI KUPITIA CCM JUN 7 MJINI DODOMA



Mpiga picha wa Chanell ten Arusha Aristrides Dotto na Elia Mbonea mwandishi wa gazeti la Mtanzania wakifanya mahojiano na Waziri wa mali asili na utalii Lazaro Nyarandu mara baada ya ibada ya jumapili katika Kanisa la KKKT Diyoyosis ya Mjini kati ambapo Waziri Nyarandu alitumia nafasi hiyo kutangaza rasmi siku atakayochukua fomu ya kuwania nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya kuwania Urais kupitia chama cha Mpindunzi.

Waziri wa mali asili na utalii Lazaro Nyarandu na waumini mbalimbali baada ya Ibada ya jumapili Jijini Arusha katika Kanisa la KKKT Diyoyosis ya Mjini Kati ambapo Waziri Nyarandu alitumia nafasi hiyo kutangaza rasmi siku atakayochukua fomu ya kuwania nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya kuwania Urais kupitia chama cha Mpindunzi .

RAIS JAKAYA AONGOZA MKUTANO WA PILI WA DHARURAWA WAKUU WA NCH WA EAC KUHUSU BURUNDI

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa kwanza kulia) kwa pamoja na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museven (wa pili kulia), Rais wa Afrika Kusini, Mhe Jacob Zuma (wa tatu kutoka kulia), Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Alain Nyamitwe (wa tatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera (wa pili kushoto), wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kabla ya kuanza rasmi kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili hali ya siasa na usalama nchini Burundi. Mkutano huo ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2015.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (wa pili kutoka kulia) akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Joyce Mapunjo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje (kulia) nao wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Dkt. Richard Sezibera akisoma maazimio yaliyofikiwa mara baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumalizika.


Kundi la Watu Maalum la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalofuatilia hali ya siasa na usalama nchini Burundi chini ya uongozi wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Sinde Warioba wakifuatilia mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini.

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, PAUL MAKONDA AFUNGUA MAONYESHO YA TANO YA SEKTA YA MAKAZI 2015


 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni kabla ya kufungua maonyesho hayo. Kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Amani Majula.


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Maonyesho ya tano ya Sekta ya Makazi kwa mwaka 2015 Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Msanifu Majengo kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba Maendeleo ya Makazi, Julius Ndege, Ofisa Mtendaji Mkuu wa EAG Group, Amani Majula waandaaji wa maonyesho hayo, Ofisa Masoko wa EAG Group, Helen Mangare na Richard Ryaganda, Ofisa Masoko wa EAG Group.

TASWIRA MBALI MBALI ZA MKUTANO WA MH. EDWARD LOWASSA WAKATI AKITANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS WA TANZANIA, JIJINI ARUSHA





Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mtangaza nia ya kuwania Urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono maelfu ya wananchi waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, wakati wa kutangaza nia yake hiyo ya kuwania Urais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mh. Lowassa akiwapungia wananchi.

Wakongwe wa Chama cha Mapinduzi walikuwepo kumpa sapoti Edward Lowassa katika safari ya matumaini pichani akiwa na mwanasiasa mkongwe mzee kingunge ngombale mwiru


Sehemu ya Mamia ya watu uliofura uwanjani hii leo.

Viongozi Mbalimbali wa Dini

Baadhi ya viongozi wastaafu kama Mzee Paul Rupia na Balozi Mwapachu nao walikuwepo

Baadhi ya Waheshimiwa Mbalimbali

Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu nae alikuwepo



Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Mh. Kangi Lugola akisalima umati wa watanzania uliofurika kwa wingi kwenye uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo, kumsikiliza Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (kulia).

Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Ndg. Onesmo Ole Nangole akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa, kwenye Uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid,jijini Arusha jioni ya leo.