Friday, April 18, 2014

MWANAJESHI FEKI AKAMATWA NCHINI KENYA AKIWA NA KITAMBULISHO NA SARE ZA JESHI

Screen Shot 2014-04-18 at 3.19.52 PM
Msahtakiwa  mwanajeshi feki bwwana Robert Mutuku.
 
Screen Shot 2014-04-18 at 3.20.16 PM 
Mtuhumiwa akiwa chini ya ulinzi
Iliwahi kutokea Tabata Dar es salaam akakamatwa askari feki wa usalama barabarani ambae ni mzee aelikua anavalia sare na madereva walikua wanajua kweli huyu ni askari na faini na rushwa akawa anazilamba kama kawaida.
Stori nyingine kwenye headlines sasa hivi ni za Mwanajeshi feki nchini Kenya ambapo kituo cha TV cha K24 ndio kimeripoti hii stori kwa kusema jamaa alishtukiwa na Mwanajeshi halisi wa nchi hiyo.
Screen Shot 2014-04-18 at 3.05.12 PM 

Huyu jamaa mwenye umri wa miaka 23 alikamatwa wakati akiwa anasafiri, anaitwa Robert Mutuku na anakiri alipata hizi jezi za jeshi kutoka kwa rafiki yake ambae alikua anamtafutia kibarua jeshini.
Akiwa tayari anashikiliwa na polisi, Mutuku ambae pia alikua na kitambulisho feki cha jeshi amekaririwa akisema ‘ni kazi nilikua naitaka ndio maana niliomba hizi nguo kwa sababu naipenda hii kazi’

No comments:

Post a Comment