Mkazi wa Mbezi-Kibanda, Andrea Marcus.
AMA kweli
ukistaajabu ya Musa utayaona ya Farao, Andrea Marcus (13), mkazi wa
Mbezi-Kibanda cha Mkaa, Dar anadaiwa kuwa wa ajabu kutokana na vitendo
vyake.
Mtoto huyu amedaiwa kuwa ni wa kichawi kutokana na maajabu yafuatayo:
Ana
uwezo wa kula ubwabwa sufuria moja la familia, anamudu kunywa maji ndoo
moja, ana uwezo wa kuingiza tumboni mikate mikubwa saba kwa mlo mmoja,
amewahi kula mchele (si ubwabwa) ndoo nzima.
Mbaya zaidi baada ya kula milo hiyo huwa haoneshi ameshiba.
Maajabu
mengine ambayo yanawashangaza watu wanaoishi naye ni jinsi anavyokula
chakula kwa kumwaga chini kisha kukomba mpaka udongo.
“Sina
amani ya moyo, naomba Watanzania wanisaidie, mwanangu ananiuma sana,
hata kujisaidia ni hapohapo, chakula anakula kupita kiasi, kama
nilivyosema hashibi na bado hali kama mwanadamu wa kawaida,” alisema
mama wa mtoto huyo.
Akizungumzia
madai ya uchawi, mama huyo, Angelina Marcus alisema mwaka 2001 alimzaa
Andrea katika mimba ya miezi nane kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Dar.
“Mama
yangu akamwambia mzazi hali kisamvu, kama anataka akanichinjie bata.
Yule mwanamke aliondoka, hakurudi tena,” alisema mama Andrea.
Aliendelea kudai kuwa, baada ya wiki tatu mtoto wake alianza tabia ya kulia usiku wa manane.
“Hiyo
tabia ya kulia amekuwa nayo miaka yote, tulikwenda kwa waganga lakini
wapi! Tukahamia makanisani kwa wachungaji kidogo mtoto alipata nafuu
mwaka jana.
“Mwezi Novemba tarehe kumi na moja, mwaka jana (2013) yule mwanamke alikuja hapa nyumbani na kuniambia kuwa, mguu ule ni wangu.
“Alikaa
chini mimi nikiwa nafua, akaanza kuniambia ‘mjukuu wangu samahani,
nimeona unateseka sana na mwanao, nataka nikurudishie kwani mimi uchawi
sasa basi.’
“Nilishtuka,
nikamuuliza bibi unasema nini? Akajibu, ‘n imekuja kukwambia huyu si
mtoto ni picha tu, mtoto wako ninaye mimi nyumbani kwangu na nina watoto
wengi ila wa kwako ananisumbua, bora uje umchukue kesho asubuhi,”
alisema mama Andrea.
“Siku
iliyofuata nilikwenda kwake, sikumwona mtoto ila cha kushangaza
aliniambia kuwa yeye anajua kuroga lakini hajui kutegua, ana mganga wake
yupo Songea (Ruvuma), atampigia simu aje amtegue mtoto wangu arudi
katika hali ya kawaida,” aliongeza mama Andrea.
Mama huyo alisema kuwa aliporudi nyumbani, aliwaambia wazazi wake kilichotokea na maneno yote waliyoongea na mwanamke huyo.
Wazazi
wa mama Andrea walimuita mwanamke huyo akiwa na mumewe na mtoto wao
mmoja, wakamuuliza kuhusu madai hayo, akaomba msamaha kwa kilichotokea.
Sakata
hilo likaenda Serikali ya Mtaa Misigani ambapo mwanamke huyo alikiri
mara ya kwanza na kusema kuwa amempigia simu mganga wa Songea atafika
wakati wowote.
“Cha
kushangaza alikaa kwa nusu saa na kusema amewapigia simu ndugu zake
wamesema huyo mganga amefariki dunia. Kila mtu alimuuliza amepigaje simu
mbona wamekaa naye na hajatoka nje? Akanyamza,” alisema mama Andrea.
Mama
Andrea alisema serikali ya mtaa waliliona sakata hilo ni kubwa na
kuamuru babu wa Andrea (jina lipo) kuchukua barua kuipeleka kwenye Kata
ili kesi ihamie huko.
Mama
huyo alimalizia kwa kusema kuwa anashindwa cha kuamua kwani kwa maelezo
ya mwanamke huyo hajui akubali mtoto Andrea si wake au la!
No comments:
Post a Comment