Zaidi
ya watu 300 bado hawajapatikana baada ya meli kubwa iliyobeba watu 459
kuzama huko South Korea ambapo sehemu kubwa ya watu waliokuwemo kwenye
meli hiyo ni wanafunzi na walikuwa wanasafiri kutoka kwenye bandari ya
Incheon kwenda kwenye kisiwa cha Jeju.
Watu watatu wamesharipotiwa kufariki licha ya watu zaidi ya 300
kutoonekana na 13 wametolewa kama majeruhi huku uokoaji zikiendelea
ambapo hadi habari hii inawekwa shughuli za uokoaji zinaendelea na watu
wengi wanaokolewa kupitia madirisha huku chanzo cha ajali kikiwa
hakijajulikana.
Meli ikiwa inaelekea kuzama kabisa
Msaada wa uokoaji unaendelea
Meli ikiwa inaza na jitihada zaukoaji kama helikopta inavyoonekana.
chanzo REUTERS.
No comments:
Post a Comment