Sunday, April 6, 2014

MELI YA CHINA YANASA SIGNAL YA NDEGE YA MALALYSIA ILIYOPOTEA

Jitihada zinaendelea kuitafuta ndege ya Malaysia MH370 iliyopotea bila kuacha alama za mojakwa moja wapi ilipo,wakati ambapo tayari serikali ya Malaysia imetangaza kuwa abiria wote watakuwa wamepoteza maisha. Wikendi hii kumekuwa na habari ya kutia matumaini baada ya maafisa wa Australia kutangaza kuwa meli ya China imenasa signal kwa mara ya pili zinazoaminika kuwa za Black Box ya ndege hiyo. Signal za kwanza zilinaswa Jumamosi. Kwa mujibu wa data hizo, meli hiyo imenasa signal ambazo zinaonekana kuwa umbali usiozidi Kilometer 2. Kiongozi wa kikosi cha anga, Angus Houston ameeleza kuwa signal hizo zimenaswa kusini mwa bahari ya Hindi na kuziita kuwa ni muhimu na zinazotia moyo katika kuongoza msako huo. Hata hivyo ametahadharisha kuwa data hizo bado hazijathibitishwa hivyo zisichukuliwe kama data sahihi moja kwa moja kuwa za ndege hiyMeli maalum ya Marekani imeelekea katika eneo hilo kuongeza nguvu. Ndege nyingine ya Australia pia imeelekea katika eneo hilo kwa mujibu wa Houston

No comments:

Post a Comment