ukiwa tuzo ya kimataifa (mwanamke mwanasiasa jasiri bora Afrika)
Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee na Mkurugenzi wa Jukwaa la
Uchumi la Dunia kwa Bara la Afrika(WEF) Elsie Kanza, ni miongoni mwa
viongozi wanawake 11 wa kisiasa kutoka barani Afrika waliotunukiwa tuzo
ya kuwa viogozi wanawake wa juu wenye nguvu katika siasa.
Mdee ambaye pia ni Waziri kivuli wa Wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi, aliunganishwa katika orodha ya wanawake jasiri katika masuala ya siasa barani Afrika kwa mwaka 2012.
Kwa mujibu wa kampuni ya Microsoft kutoa Marekani inayojihusisha na masuala ya Kompyuta iliyoandaa tuzo hizo, Mdee na Kanza ni miongoni mwa viongozi jasiri katika masula ya siasa kutoka barami Afrika ambao wanahitaji kupongezwa.
“Mwaka 2012 ulikuwa mwaka mzuri kwa viongozi wanawake wa kisiasa pamoja na marais wawili wanawake na viongozi wawili wanawake kutoka Umoja wa Afrika, Microsofti iliangalia wanawake 11 ambao wako makini katika masuala ya siasa barani Afrika,” ilieleza sehemu ya maelezo yaliyowekwa kwenye mtandao.
Wengine waliotunukiwa ni Rais wa Malawi, Joyce Banda; Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf; Mbunge kutoka Kenya, Charity Ngilu; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda, Louise Mushikiwabo na Waziri wake wa Afya, Agnes Binagwaho.
Wengine ni Rais wa Muungano wa Afrika, Nkosa Zana Dlamini Zuma; Waziri wa Fedha wa Nigeria, Ngozi Okojo-Iweala; Makamu wa Rais wa Zimbabwe, Joyce Mujuru na Mwenyekiti wa chama cha CPPG cha Ghana, Samia Nkhrumah

GREDIT JAMIIFORUM
No comments:
Post a Comment