Napenda nichukue fursa hii kutoa ufafanuzi wa taharuki iliyotokea
jana tarehe 02 Januari, 2015 katika jiji la Dar es Salaam ikiwahusisha
baadhi ya vijana wanaojikusanya kwenye vikundi na kujiita Panya road na
pengine kusababisha hofu kubwa kwa wananchi.
Chanzo cha taharuki hiyo, kulitokana na kuuawa kwa kijana mmoja
ajulikanae kwa jina la Mohamed Ayub na wananchi tarehe 01/01/2015 katika
maeneo ya Tandale kwa Mtogole kwa tuhuma za wizi wakati wa mkesha wa
sikukuu ya mwaka mpya. Tarehe 02/01/2015 majira ya saa tisa mchana
yalifanyika mazishi ya kijana huyo katika makaburi ya Kihatu Kagera
Mikoroshini na taarifa zilizokuwa zimelifikia Jeshi la Polisi Kanda ya
Dar es Salaam ni kwamba baada ya mazishi hayo vijana wenzake na marehemu
walijipanga kufanya fujo ili kulipiza kisasi cha mwenzao kuuawa. Aidha,
kabla vurugu hizo hazijafanyika na kwa vile Polisi walishaona dalili ya
vurugu hizo, tayari walifanikiwa kuzidhibiti.
Baada ya vurugu hizo kudhibitiwa na Polisi, vijana hao walitawanyika
kwa kukimbia katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na kuzua
taharuki kubwa kwa wananchi kwamba huenda kila walipokimbilia wanampango
wa kuwafanyia fujo raia wema, jambo ambalo wasingeweza kulifanya kwa
vile Polisi walikuwa wameimarisha ulinzi katika maeneo yote ya jiji.
Kufuatia hali hiyo na Jeshi la Polisi nchini likiwa linaendelea na
msako mkali wa kuwabaini na kuwakamata wote wanaojihusisha na uhalifu
huo, tunawaomba wananchi watulie, wasiwe na hofu na waendelee na
majukumu yao kama kawaida. Mpaka sasa tunawashikilia watuhumiwa 36 kwa
mahojiano na uchunguzi utakapokamilika tutawafikisha mahakamani mara
moja.
Aidha, Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa vijana hao wananojihusisha na vikundi hivyo kuacha tabia hiyo mara moja. Tumejipanga vizuri katika mikoa yote kuhakikisha kwamba nchi inaongozwa kwa kufuata utawala wa sheria, hatutamwonea muhali mtu yeyote ama kikundi cha watu wanaotaka kuvuruga amani ya nchi na kutia hofu wananchi.
Wananchi waendelee kutupa ushirikiano kwa kutoa taarifa kupitia namba ya simu 0754 78 55 57, namba za makamanda au katika kituo chochote cha Polisi.
Imetolewa na:-
Advera John Bulimba - SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

No comments:
Post a Comment