Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amemsifu mshambuliaji wake Ddier
Drogba kwa kusema kuwa bado kuna mengi ya kutegemewa toka kwa mchezaji
huyo na hajaisha kama inavyodhaniwa na wengi .
Mourinho alisema hayo kwenye hafla maalum ya utoaji wa tuzo ya
heshima kwa Dorgba ambayo iliandaliwa na chama cha waandishi wa habari
za michezo nchini England .
Hafla hiyo iliyoandaliwa na waandishi ililenga kumtunukia tuzo ya
heshima mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast kwa mchango wake kwenye
mchezo wa soka na kwenye ligi ya England kwa jumla
Mourinho alimsifu Dorgba akimuita mchezaji mwenye thamani ya kipekee
kwa timu hiyo baada ya mchango wake kuipa mafanikio mbalimbali tangu
alipojiunga nayo mwaka 2004 wakati aliposajiliwa toka Olympique Marseile
.
Tuzo kama hii imewahi kutolewa kwa kocha Jose Mourinho na Sir Alex
Fergusson pamoja na wachezaji kama David Beckham baada ya mafanikio ya
muda mrefu .
Drogba mwenyewe kwa upande wake aliishukuru klabu ya Chelsea kwa
kumpa nafasi ya kupata mafanikio ambayo labda asingeyapata kwenye klabu
nyingine na akasisitiza kuwa ataendelea kuwa sehemu ya familia ya
Chelsea kwa muda mrefu ujao .
Mourinho ameonyesha dhamira ya kutaka kuendelea kuwa na mchezaji huyo
kwa ajili ya msimu ujao baada ya kusema kuwa kuna mengi ya kutarajiwa
toka kwa Drogba na watu hawapaswi kudhani kuwa ameisha na anangoja
kustaafu .
No comments:
Post a Comment