Katika kikao chake na waandishi wa habari mchana huu katika hotel ya
Snowcrest jijini Arusha, Lema amesema anaenda kupambana na Iddi Azan
kwenye jimbo la Kinondoni ktk uchaguzi mkuu ujao mwezi October mwaka
huu. Akielezea nia yake hiyo mbele ya mamia ya waandishi wa habari, Lema
amesema anataka kuleta mapinduzi ya fikra kwa wana kinondoni na
kuijenga ngome imara ya chadema jimboni hapo. Alisema mpango wake huo
alikuwa nao toka mwaka 2013 pale alipovuliwa ubunge na alitafakari
kujiingiza kwenye changamoto mpya kisiasa ifikapo mwaka 2015.
“Wana wa Arusha wasiwe wanyonge, kamanda wao naenda kupambana kwenye
uwanja mwingine wa vita lakin wajue tupo pamoja” Alinukuliwa akisema bw.
Lema. Hata hivyo alikwepa kujibu swali la mwandishi wa Radio 5
aliyetaka kujua kama pengine ni mbinu ya Lema kukwepa aibu ya kushindwa
kwenye uchaguzi huu ikizingatiwa historia yake tata ya utekelezaji wa
ahadi zake alizotoa mwaka 2010 na pia ushindani mkali unaomkabili ndani
ya chama chake. Imefahamika kuwa wanachama zaidi ya 30 wameshatangaza
waziwazi kuchuana na Lema kwenye uchaguzi wa Octoba.
Hii inaweza kuwa ni mbinu ya Lema kukimbia changamoto na kujaribu karata yake mahali pengine
Hii inaweza kuwa ni mbinu ya Lema kukimbia changamoto na kujaribu karata yake mahali pengine
No comments:
Post a Comment