Pages

Thursday, July 17, 2014

USIKU WA MATUMAINI 2014 ALI KIBA: NITAMKALISHA YEMI ALADE TAIFA


 
Ally Saleh ‘Ali Kiba’
 MFALME wao Bongo, Ally Saleh ‘Ali Kiba’ amefunguka kuwa ataiandika historia ya aina yake kwa kumuonesha mkali wa songi la Johnny, Yemi Alade kutoka Nigeria jinsi gani muziki unatakiwa kuimbwa na kuchezwa.
Mpango mzima utakuwa ni Agosti 8, mwaka huu wakati Tamasha la Usiku wa Matumaini litakapokuwa likichukua nafasi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar ambapo Kiba pamoja na listi kibao ya wasanii itahusika kulipamba tamasha hilo.
Akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo kubwa lenye lengo la kudumisha amani na upendo miongoni mwa Watanzania, Ali Kiba alisema anatambua kuwa ni muda mrefu mashabiki wamekuwa na hamu kumuona akipafomu, hivyo siku hiyo atashuka na sapraizi kibao ambazo hajawahi kuzionesha.
“Ukiachana na kupiga nyimbo zangu zote kali siku hiyo jukwaani, nitawaonesha sapraizi kubwa mashabiki, huyo Yemi lazima akae.

“Shoo zangu huwa sibahatishi hata siku moja, nitaimba na kucheza sambamba na mashabiki kibao watakaofurika uwanjani hapo,” alisema Ali Kiba.Mwanadafada Yemi Alade amesema mbali na kupiga shoo matata, siku hiyo atamtafuta Johnny ambaye alimuimba katika wimbo huo na akimpata atarudi naye Nigeria.
Kwa kujibu wa mratibu wa tamasha hilo, Luqman Maloto, utamu wa tamasha hilo hautaishia hapo kwani mastaa wa filamu, Jacqueline Wolper na Irene Uwoya wataonesha upande wa pili wa maisha yao kwa kupanda ulingoni na kuzipiga kumtafuta mshindi.
Maloto aliongeza kuwa, mbali na ndondi hizo, kutakuwa mechi kati ya Timu ya Bongo Fleva na Bongo Movie. Mwaka jana walishinda Bongo Fleva na mwaka huu Bongo Movie wanataka kulipiza kisasi.
 
Yemi Alade
Listi haikuiishia hapo kwani Maloto alisema kutakuwa na mechi kati ya Wabunge mashabiki wa Simba dhidi ya wenzao wa Yanga, ngumi kati ya mabondia Thomas Mashali na Mada Maugo, Khalid Chokoraa na Said Memba huku mheshimiwa Mwigulu Nchemba akizichapa na Dk. Hamis Kigwangala.
Aidha, Maloto aliweka plain kuwa mastaa watakaolishambulia jukwaa siku hiyo ni pamoja na R.O.M.A Mkatoliki, Madee, Juma Nature na kruu nzima ya Wanaume Halisi na wengine kibao ambao watatajwa hapo baadaye.
Sehemu ya mapato inayopatikana katika tamsha hilo inapelekwa katika Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule za sekondari nchini.
Mpango mzima wa tamasha hilo umepigwa tafu na  Kampuni ya Vodacom, Pepsi, Azam TV, E. FM, Clouds FM na Times FM.

credit gpl

No comments:

Post a Comment