Kiba ambaye ni mkongwe kunako muziki wa Bongo Fleva, amefunguka yeye
siku zote ni staa na huwa hakosei hivyo mashabiki watarajie burudani
kali siku hiyo.
Kiba ameizungumzia shoo yake katika tamasha hilo kwamba itakuwa spesho hivyo mashabiki wategemee mambo yafuatayo;

Shoo kali
Katika shoo zake zote huwa habahatishi. Amekuwa ni msanii wa kwanza kutoka Bongo kwa kupiga idadi ya shoo nyingi nje ya nchi kuliko msanii yeyote hata katika matamasha ya ndani ya Bongo amekuwa akiteka hisia nyingi za mashabiki, kwenye Tamasha la Matumaini amesema itakuwa ni zaidi ya burudani.

Ali Kiba’ akipozi.
Kuchomoka kivingine
Baada ya kukaa kimya kwa muda sasa mfalme huyo mwenye sauti ya ajabu, sauti ya kumfanya kila shabiki aikumbuke inapopotea kidogo, amesema anakuja kivingine ambapo atapiga muziki wake kwa mpangilio maalum kuanzia sauti nzuri ya kuwabembeleza.

Habakishi kitu
Kiba amesema siku hiyo hatabakisha kitu, atazipiga nyimbo zote kali kuanzia zile za zamani kama Single Boy, Dushelele, Mac Muga, Run Dunia na nyingine kibao bila kusahau Mwana na Kimasomaso ambazo ndiyo habari ya mjini.

Tamasha hilo linatarajiwa kupambwa na matukio kibao ya kusisimua kama
ngumi za wabunge, mechi za mpira wa miguu za wabunge na wasanii wa
Bongo Fleva, Bongo Movie bila kusahau burudani nzuri kutoka kwa wasanii
wanaotamba katika muziki wa Injili.
Burudani zote hizo kwa pamoja, mashabiki watazishuhudia kwa mtonyo wa
shilingi elfu tano tu huku sehemu ya mapato yatakayopatikana ikipelekwa
katika mfuko wa elimu nchini
No comments:
Post a Comment