Waumini wakiendelea na usafi kabla ya kiongozi wao kupita.
Ripota
wa TZA nchini Kenya Julius Kipkoitch anaripoti kwamba wakazi wa jiji la
Eldoret wamemfanya kila alieiona hii kuvutiwa na pengine kujua imekuaje
wakafanya hivi kwa mara ya kwanza baada ya kujitosa na kupiga deki
barabara ya lami ya Oginga Odinga jijini Eldoret kaunti ya Uasin Gishu
nchini Kenya.
Unaambiwa wameamua kufanya hivi ikiwa ni maandalizi ya kumlaki
nabii Daktari Awuor kwa ajili ya maombi ya leo na siku ya Jumatatu
kuadhimisha pasaka na kumshukuru jehova kwa kuwasaidia jiji la Eldoret
kufanyika uchaguzi wa amani mwaka 2013
Hata hivyo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii maoni yalikotolewa
na Wakenya kuhusu hii ishu, maoni mengi yameonekana kupinga kitendo cha
waumini hao wa kanisa la Jesus is lord kwa kumpa Daktari Awuor heshima
kupita kiasi.CREDIT; MILLARDAYO
No comments:
Post a Comment