Wote
tunafahamu kwamba rapper 50 cent anajua kutumia fursa za kuweza
kujitengenezea fedha. Lakini safari hii biashara zake zimemletea
matatizo kupitia kesi iliyodumu kwa miaka 3 kati yake dhidi ya kampuni
ya kutengeneza earphone – Bradenton.
Kwa mujibu wa mtandao wa www.hot97.com, ni kwamba 50 Cent ameamriwa
na mahakama kuilipa kampuni hiyo kupitia kitengo chake Sleek Audio
karibia $4.5 million kama fidia ya malipo mwanasheria na $11.7 million
kama fidia ya kuvunjika kwa mkataba na kampuni hiyo ambayo ilikuwa
wakishirikiana kutengeneza 50 Cent headphones.
50 Cent mwanzoni alituhumiwa kuiba designs za Sleek Audio, ambazo
mwanzoni alipewa kwa ajili kuzipitisha kwa ajili ya kuanza kwa
uzalishaji wa headphones hizo, lakini baadae 50 aliwageuka Sleek na
akaamua kushirikiana na kampuni nyingine kutumia designs alizopewa na
kampuni ya Sleek.
No comments:
Post a Comment