Sunday, March 2, 2014

G7 YAILAANI URUSI KUHUSU UKRAINE

 
Maandamano ya kuipinga Urusi, Ukraine.
Kundi la mataifa saba yaliyostawi zaidi kiviwanda almaarufu kama G7 limelaani vikali hatua za kijeshi zilizochukuliwa na Urusi nchini Ukraine-viongozi kundi hilo wakitaja hatua ya Urusi kama ukiukaji wa uhuru wa Ukraine.
Katika taarifa ya pamoja iliyotiwa pia saini na Umoja wa Ulaya EU-Urusi imetakiwa kushughulia wasiwasi wake kuihusu Ukraini kupitia mashauri au upatanishi.
Kundi hilo la mataifa saba tajiri zaidi duniani maarufu kama G-Seven limesema kuwa linachukuwa uamuzi wa kuahirisha matayarisho ya kongamano ambalo lingefanyika nchini Urusi mwezi juni mwaka huu kutokana na vitendo vya Moscow. Taarifa hiyo inakuja wakati vikosi vya Urusi vikiimarisha uthibiti katika rasi ya crimea ambapo Urusi inasema kuwa inalinda raia wake baada ya serikali kupinduliwa mjini Kiev.
Mbunge mashuhuri wa Urusi - Vyacheslav Nikonov, ameimabia BBC kwamba Urusi imejiandaa kwenda vitani kulinda maslahi yake nchini Ukraine na hususan katika mji wa Sevastopol.
"Ukraine ilialikwa kujiunga na Nato na hii ina maana kuwa marekani, au vituo vyake vya kijeshi vitawekwa nchini Ukraine. Urusi itafanya lolote, itahatarisha kuingia vita kuzuia hilo kutokea. Ni kuhusu kituo cha kijeshi, ni kuhusu mustakabal wa Urusi, mustakabal wa Ukraine. Sidhani kama mataifa ya magharibi yanaelewa kwamba Ukraine ni mahali ambapo Urusi ilizaliwa," amesema Nikonov.


Wanajeshi wasiotambuliwa washika doria katika kambi moja ya kijeshi nchini Ukraine.
Awali serikali ya mpito ya Ukraine iliishutumu Urusi kwa kutangaza vita na kuwaamuru wanajeshi wake kuwa tayari kwa makabiliano.Shirika la kujihami kwa mataifa ya Magharibi NATO limetowa wito kwa Urusi kuwaondoa wanajeshi wake nchini Ukrainena kuzitaka pande zote kusuluhisha mgogoro huo kwa njia ya amani. Taarifa hiyo imetolewa baada ya mkutano wa dharura wa mabalozi wa NATO mjini Brussels kujadili mgogoro huo. Katibu mkuu wa NATO, Anders Fogh Rasmussen, amesema kuwa huenda wachunguzi wa umoja wa mataifa wakatumwa kusaidia kusuluhisha hali ya mambo.
"Tunatoa wito kwa urusi kuheshimu ahadi zake za kimataifa, kuondoa vikosi vyake na kujiepusha na uvamizi katika maeneo mengine nchini Ukraine. Tunatowa wito kwa pande zote kufuata njia ya amani katika kusuluhisha mgogoro huo kupitia mazungumzo, kupitia wachunguzi wa kimataifa chini ya mwavuli wa umoja wa baraza la usalama la umoja wa mataifa au shirika la ushirikiano wa kiusalama ulaya OSCE,'' amesema bwana Rasmussen.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa marekani , John Kerry, anatarajiwa kuzuru Kiev hapo kesho jumanne kuiunga mkono serikali mpya ya Ukraine.
Haya yanajiri wakati mkuu wa jeshi la wanamaji wa Ukraine, Denis Berezovsky, akipokonywa madaraka yake baada ya kusema hadharani kwamba anaunga mkono serikali mpya ya Jimbo la Crimea ambayo inaunga mkono Urusi. Serikali ya Kiev imesema kuwa inamfanyia uchunguzi kwa nia ya kumfungulia mashtaka ya uhaini.

KAMPENI ZAZIDI KUPAMBA MOTO KALENGA

Meneja Kampeni wa Chama cha Deokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Alphonse Mawazo, akicheza ngoma ya jamii ya kimasai baada ya kufanya kampeni ya nyumba kwa nyumba kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Grace Tendega Mvanda, jana asubuhi

Mzee wa Mila wa Kimasai katika Kijiji cha Mfyome, Lioper Ilmuduji, akimpatia baraka mgombea ubunge  wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Bi. Grace Tendega Mvanda, wakati chama hicho kilipofanya kampeni ya nyumba kwa nyuma kuomba kura kwa wananchi katika kijiji hicho jana asubuhi.

. Mgombea ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Bi. Grace Tendega Mvanda akishiriki chakula cha kimila pamoja na watu wa jamii ya kimasai katika Kijiji cha Mfyome jana asubuhi baada ya msafara wa mgombea huyo kufika kijijini hapo kufanya kampeni za nyumba kwa nyumba.
Mgombea Ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi mdogo Jimbo la Kalenga, Grace Tendega Mvanda, akizungumza kuomba kura wakati chama hicho kilipofanya kampeni ya nyumba kwa nyumba na mtu kwa mtu katika Kijiji cha Mfyome, jana asubuhi

MANCHESTER CITY MABINGWA CAPITAL ONE

Yaya Toure wa Manchester City akishangilia goli
Timu ya Manchester City ni wameibuka mabingwa wa kombe la Capital One baada ya kuwabwaga Sunderland magoli 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa uwanja wa Wembley, Jumapili.
Sunderland ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na mshambuliaji wake Fabio Borini katika dakika ya kumi ya mchezo.

KURA YA SIRI: ESTHER BULAYO, ANA KILANGO NA PROF KAPUYA WATOFAUTIANA NA MSIMAMO WA CHAMA CHAO.

Mbunge wa viti maalum kutoka mkoa wa Mara, Wajumbe watatu wa Bunge la Katiba ambao ni wabunge wa CCM wametofautiana na msimamo wa chama chao kwa kuunga mkono kura ya siri itumike kuamua ibara za Rasimu ya Katiba.Hilo lilitokea jana katika mjadala mkali baina ya wajumbe kuhusu ama matumizi ya kura za siri yatumike au kura za wazi.
Katika mjadala huo ulioonyesha mgawanyiko wa wazi, wajumbe wengi wanaotokana CCM na ambao wamekuwa wakipigania kura za wazi, walionekana kuwazidi kwa wingi wale wanaotaka kura za siri.
Wajumbe wa CCM ambao ni wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muunganom– Esther Bulaya na Profesa Juma Kapuya walijitoa mhanga na kueleza bayana kuwa hawako tayari kuona demokrasia ikikandamizwa kwa kulazimishwa kupiga kura za wazi. Akishangiliwa kwa nguvu, Bulaya alisisitiza kuwa hayuko tayari kulazimishwa kupiga kura ya wazi huku akijua kuwa utaratibu huo unamnyima uhuru wake.
“Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko. Ni lini na wapi maamuzi magumu kama haya yalifanyika?” Alihoji mbunge huyo wa Viti Maalumu.
Bulaya alisema hakuna sheria inayomtaka mtu kushurutishwa kufanya uamuzi na kwamba kumtaka atoe sauti ya juu katika kura za wazi, ni kumlazimisha kufanya kinyume na matakwa yake.
Alisema kamwe hawezi kuuza uzalendo wake kwa kupiga kura za wazi na kwamba atapimwa kwa utashi wake kuhusu kile anachokiamini. Kwa upande wake, Profesa Kapuya alisema namna nzuri ya kumpa uhuru mpiga kura, ni kutomshurutisha ili afuate matakwa ya wengine.
Alisema kura za siri ndizo zitakazowaimarisha wajumbe na kwamba kinyume chake, kura za wazi zitawagawa na hatimaye kutoka bungeni wakiwa vipande vipande.
Kwa upande wake, Anna Kilango Malecela aliunga mkono ‘kiaina’ kura ya siri akisema alimsikiliza Profesa Ibrahim Lipumba kwa karibu saa nzima kupitia Kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC), akamshawishi kutokana na hoja alizozitoa.
Alisema kwa kuwa suala hilo limezua mvutano mkubwa katika bunge hilo, ni bora likaamuliwa kwa kupigiwa kura ya siri.
Wajumbe wengine
Mjumbe wa Bunge hilo, Sheikh Mussa Kundecha aliunga mkono utaratibu wa kura ya siri akisema ndiyo pekee unaoweza kuwaunganisha wajumbe.
Mchungaji Christopher Mtikila alitumia dakika tano kutoa somo kwa wajumbe wa Bunge hilo, kuhusu umuhimu wa kupiga kura ya siri badala ya kura ya wazi.
“Mwenyekiti, wewe tumekuchagua kwa kura ya siri siyo kwamba tulikuwa wajinga kuliko wenzetu, hapana! Ni democratic civility (ustaarabu wa kidemokrasia),” alisema.
Mjumbe mwingine, Philemon Ndesamburo aliwataka wajumbe kuacha ushabiki wa kisiasa na kwamba lazima wazingatie kwamba wanatengeneza Katiba itakayodumu kwa miaka 50 au miaka 100 ijayo. Hata hivyo, wajumbe, Sixtus Mapunda na Stephen Wassira wote wa CCM, walisema kura za wazi ndiyo suluhisho la kutoa uamuzi juu ya nani anasema nini na kwa wakati gani.
Dk. Zainabu Gama alisema baadhi ya watu wanaotaka kura za siri wametumwa au wamekula rushwa ndiyo maana hawataki kura za wazi.
Wassira alikiri kuwa CCM imeingia na msimamo ndani ya Bunge, lakini alisema hata wajumbe wengine pia wana misimamo yao.
Chanzo: Mwananchi

CHADEMA Vs CCM KIMENUKA KALENGA-IRINGA.

Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Salum Mtenga akimnadi mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa katika Kijiji cha Ilala Simba
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amewataka wananchi wa Jimbo la Kalenga mkoani hapa kutambua kuwa chama hicho kipo kwa lengo la kuwatetea wananchi bila kujali itikadi za vyama 
Iringa. Naibu Katibu Mkuu wa (CCM)-Bara, Mwigulu Nchemba amewataka wananchi wa jimbo hilo kumchagua Mgombea wa Chama hicho, Godfrey Mgimwa ili awaletea maendeleo yanayotokana na utekelezaji wa ilani ya chama hicho tawala.
Wakati CCM ikisema hayo, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) John Heche amesema, chama hicho kitasimamia maoni ya wananchi yaliyomo katika Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba.
Akizungumza jana kwenye kampeni za uchaguzi katika Kijiji cha Magubike na Nzihi Kata ya Nzihi, Nchemba ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha alisema, anayeweza kusimamia utekelezaji wa ilani hiyo ni Godfrey Mgimwa kutoka CCM.
Aliwataka Wanakalenga kuchagua mbunge anayetokana na CCM ili kuendeleza na kukamilisha miradi ya umeme na maji ambayo imeanza kutekelezwa tangu 2010.
Alisema Wanakalenga wakimchagua mbunge kutoka chama cha upinzani, wataendelea kupata shida zikiwamo za kukosa maji na umeme
Naye Godfrey Mgimwa aliwaomba Wanakalenga kumpa kura za ndiyo ili aweze kuungana na wabunge wengine katika kupeleka maendeleo katika jimbo hilo lenye changamoto nyingi za elimu, afya na mawasiliano.
Alisema yeye siyo mzungumzaji, bali ni mtendaji na kuwa atafanya mambo mengi ikiwamo kutekeleza ahadi ambazo baba yake alikuwa bado hajazitekeleza za madawati na uchangiaji wa ujenzi wa zahanati na shule katika Kata za Kalenga.
Katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Ipamba, Heche alisema, wameanza mchakato wa katiba kwa gharama kubwa, huku akishangazwa na hatua ya CCM kuandaa waraka unaobadili mambo yote muhimu yaliyoandikwa katika Rasimu hiyo na Tume ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa Jaji Joseph Warioba.
Alitaja moja ya sababu ya chama hicho kuwataka wamchague mgombea ubunge kupitia Chadema kuwa, CCM imeshindwa kuwaletea maendeleo kwa zaidi ya miaka 50 tangu uhuru.
“Kila wakati wa uchaguzi, CCM huja na kutoa ahadi lukuki kuwa tutawaletea maji, barabara, huduma za afya...leo viko wapi? Tunaomba mumchague Grace, mjaribuni ili awaletee maendeleo,” alisema Heche.
Naye, Grace aliwataka wananchi hao kumchagua ili aende kukomesha vitendo vya manyanyaso ya michango mbalimbali kutoka kwa Serikali.

Saturday, March 1, 2014

LIGI KUU ENGLAND:CHELSEA,LIVERPOOL,EVERTON NA STOKECITY ZA SHINDA

Andre Schurrle: Mchezaji wa Chelsea aliyefunga goal thidi ya Fulham
Andre Schurrle's amefunga kwa hat-trick nakusababisha Chelsea kupata points 4 zaidi ya Liverpool na Arsenal na kuiwaka kileleni mwa ligi ya England

Moussa Sissoko alipata magoli katika kipindi cha kwanza na cha pili cha mchezo kupelekea Newcastle kushinda dhidi ya Hull City kwa magoli 4 kwa1 katika uwanja wa KC Stadium,

Haya ni matokeo ya mechi za jana
Everton 1Westham o
Fulham1 chelsea 3
Hulcity1 Newcastle 4
Stoke1 Arsenal 0
Southampton 0 Liverpool 3








































































































































JESHI LA URUSI LARUHUSIWA KWENDA CRIMEA

Bunge la Crimea linapepea bendera ya Urusi
Bunge la Urusi limeidhinisha ombi la Rais Putin kuwa wanajeshi wa Urusi watumike Ukraine.
Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Urusi imesema hiyo haimaanishi kuwa wataanza kutumika moja kwa moja, ingawa wakuu wa Ukraine wanasema Urusi imeshatuma wanajeshi 6,000 zaidi huko Crimea.
Kikosi cha wanamaji wa Urusi katika Black Sea kimesema kuwa wanajeshi wake wanapiga doria pamoja na wenyeji wa Crimea wanaounga mkono Urusi, ili kulinda vituo vyake.
Mwandishi wa BBC alioko Sevastopol anasema wanajeshi wanaonekana zaidi.
Meli za Ukraine za kulinda pwani zimeondoka kuepuka kuchukuliwa na Urusi na mwandishi wa BBC anasema kuna hisia kuwa ras wa Crimea inazidi kuwaponyoka wakuu mjini Kiev.

MTOTO WA RAIS MORSI AKAMATWA.

Watoto wa Morsi

Shirika la habari la Misri linasema kuwa kitinda mimba wa rais aliyeondolewa madarakani, Mohamed Morsi, amekamatwa akishukiwa alikuwa na dawa ya kulevya.
Shirika la habari la taifa linaarifu kuwa polisi walikagua gari walilokuwa na shaka nalo na ndani walimkuta Abdullah Morsi na rafiki.
Inaarifiwa kuwa ndani ya gari piya zilikutikana sigara mbili zilizokuwa na bangi.
Mtoto mwengine wa kiume wa Mohamed Morsi amelaani kukamatwa kwa ndugu yake, na kusema kuwa mdogo wake amesingiziwa tu.
Mohamed Morsi mwenyewe hivi sasa anakabili kesi nne za mashtaka ambayo adhabu yake inaweza kuwa kifo.

YANGA YAICHAKAZA AL AHLY 1-0

MAF3Klabu bingwa ya Tanzania bara Dar Young Africans leo imefanikiwa kushinda mchezo wa kwanza wa hatua ya raundi ya pili CAF Champions League dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe hilo Nacional Al Ahly ya Egypt.
Mchezo huo uliopigwa katika dimba la uwanja wa taifa Dar es Salaam uliotawalia kwa kiasi kikubwa na Yanga ambao walipoteza nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza na mpaka timu zinaenda mapumziko hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzie.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa upande wa Yanga walionekana kutafuta bao kwa nguvu, mpaka kufikia dakika ya 50 tayari walishapata kona tisa ambazo hazikuzaa matunda. Wakati muda ukizidi kuyoyoma na mashabiki wa Yanga wakiwa wameanza kukata tamaa ya kupata ushindi dhidi ya waarab, Nadir Haroub Cannavaro aliwainua maelfu ya mashabiki wa Yanga katika dakika ya 82 baada ya kuipatia timu yake bao la kuongoza.
Mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho ubao wa matokeo ulikuwa unasomeka 1 kwa upande wa yanga na 0 kwa waarabu. Timu hizi zitarudiana jijini Cairo wiki mbili zijaz

SPOTS! UEFA YA YAMPA AZABU PELLEGRINI



Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini
Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini amepigwa marufuku mechi mbili na UEFA asisogelee eneo la kiufundi la uwanja kwa kumlaumu mwaamuzi baada ya klabu yake kushindwa na Barcelona katika michuano ya klabu bingwa ya Ulaya.
Pellegrini alisema baada ya timu yake kushindwa 2-0 nyumbani kwamba mwaamuzi kutoka Sweden Jonas Eriksson "hakua mwaadilifu kwa timu zote mbili".
Alituhumiwa kwa ukosefu wa nidhamu na amepewa adhabu ya kukaa jukwaani pamoja na mashabiki katika mkondo wa pili wa mchuano na Barcelona mnamo Machi 12 March, poja na Mechi nyingine za ziada.
Adhabu ya mechi moja nyingine imesimamishwa kwa miaka miwili.

OBAMA AIONYA URUSI KUHUSU UKRAINE


Rais Barack Obama wa Marekani

Rais Barack Obama wa Marekani ameionya Urusi, kuwa hatua yoyote ya kuingilia kijeshi mgogoro wa Ukraine itakuwa na madhara makubwa.

Bwana Obama amesema amesikitishwa na taarifa za kuwepo harakati za majeshi ya Urusi nchini Ukraine.
Kaimu rais wa Ukraine,Olexander Turchynov, ameishutumu Urusi kwa kupeleka vikosi vyake katika jimbo la Crimea nchini Ukraine ili kutaka kuibua "mgogoro wa kijeshi".
Waziri mkuu wa Crimea anayeipendelea Urusi, ameiomba serikali ya Urusi kusaidia kuimarisha amani katika jimbo hilo.
"Namwomba rais wa Shirikisho la Urusi, Vladimir Putin, kutoa msaada ili kuimarisha amani na utulivu katika jimbo la Crimea lenye mamlaka ya kuijiamulia mambo yake lenyewe." Amesema Bwana Serhiy Aksyonov katika taarifa.
Bwana Aksyonov, ambaye aliteuliwa na bunge la Crimea siku ya Alhamisi, pia amesema anashikilia kwa muda wizara ya mambo ya ndani ya Crimea, majeshi, usafiri na ulinzi wa mipaka.
Tangu kuondolewa madarakani kwa Rais Victor Yanukovych wa Ukraine ambaye kwa sasa yuko uhamishoni nchini Urusi, mgogoro umehamia katika jimbo la Crimea, ambalo wakaazi wake ni Warusi.

MTUHUMIWA WA UGAIDI AKAMATWA UINGEREZA

 
Moazzam Begg, mtuhumiwa wa ugaidi

Mfungwa wa zamani katika gereza la Guantanamo Bay,Moazzam Begg na mwananmke mmoja mwenye umri wa miaka 44 wamefunguliwa mashitaka yanayohusiana na makosa ya ugaidi nchini Syria.
Polisi wa West Midlands nchini Uingereza wamesema Bwana Begg, mwenye umri wa miaka 45, mkaazi wa Hall Green, Birmingham, ameshitakiwa kwa kutoa mafunzo ya kigaidi na kufadhili ugaidi nje.
Mwanamke anayeshitakiwa pamoja naye, Gerrie Tahari, wa Sparkbrook, Birmingham, anashitakiwa kwa kufadhili ugaidi nje ya nchi.
Watuhumiwa hawa watafikishwa mbele ya mahakama ya Westminster Jumamosi.
Watuhumiwa hao wawili walikamatwa Jumanne. Watu wengine wawili walikamatwa siku hiyo na kuwekwa mahabusu.
Watuhumiwa hao, mmoja mwenye umri wa miaka 36 anatoka eneo la Shirley, Solihull, na mwenye umri wa miaka 20 anatoka Sparkhill, Birmingham, ambao wanashikiliwa kwa tuhuma za kufadhili vitendo vya kigaidi nje.
Bwana Begg alikuwa akishikiliwa katika gereza la Marekani lililoko Guantanamo Bay nchini Cuba kwa karibu miaka mitatu.
Ni raia wa Uingereza ambaye alihamia Afghanistan pamoja na familia yake mwaka 2001, kabla ya kwenda tena Pakistan mwaka 2002 wakati vita vya Afghanistan vilipoanza.
Alikamatwa mjini Islamabad Januari 2002 na kupelekwa katika kituo cha Bagram nchini Afghanistan kwa karibu mwaka mmoja na baadaye kuhamishiwa Guantanamo.
Aliachiliwa mwezi Januari 2005 pamoja na raia wengine watatu wa Uingereza na kurejea Uingereza.
Bwana Begg, ambaye kwa sasa anaongoza kampeni ya kusaidia familia za watu wanaoshikiliwa magereza, hakuwahi kushitakiwa kwa kosa lolote.

AIRTEL KUZAMINI TUZO YA MWANAMAKUKA 2014



Airtel yadhamini Tuzo ya Mwanamakuka 2014

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza kudhamini tuzo za Mwanamakuka zenye lengo la kusaidia wanawake kutoka katika maeneo mbalimbali kujiinua kiuchumi
Tuzo za Mwanamakuka zinaandaliwa na The Unity of Women friends kila mwaka zikiwatambua wanawake jasiri waliopambana kubadili maisha yao kutoka katika hali ngumu, duni na umaskiniAkiongea kuhusu udhamini wa Tuzo hizo Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” Airtel inaamini kwamba ujasiriamali ni muhimu katika kufikia maendeleo ya kiuchumi na kuondoa umaskini. Kwa kudhamini tuzo hizi za mwanamakuka tunajikita katika kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi na kuwa sehemu ya shughuli za maendeleo ya wanawake nchini”.
Kwa miaka mitatu mfululizo Airtel tumekuwa moja ya wadhamini wa tuzo hizi za mwanamakuka ambazo zimebadili maisha ya wanawake na kuwawezesha kuwa wafanyabiashara wenye mafanikio. Tutaendelea kuonyesha dhamira yetu katika mipango ambayo itasaidia wanawake walio katika mazingira magumu kujikwamua kiuchumi na kukuza maendeleo ya taifa."Jane aliongeza kwa kusema , kuna msemo unaosema ukimwezesha mwanamke umewezesha jamii nzima. Airtel tumejipanga kuwawezesha wanawake kiuchumi kwani tunaamini kwa kufanya hivyo tutakuwa tumewezesha jamii kwa ujumla
Kwa upande wake mwenyekiti na Mratibu wa Mradi wa The Unity of Women friends Maryam Shamo alisema” Tunashukuru Airtel kwa kushirikiana nasi katika kufanikisha tuzo hizi ambazo ushirika huu umekua wa mafanikio makubwa. Lengo la tuzo hizi ni kuwahamasisha na kuwavutia wanawake kufikia ndoto zao. Lakini hasa tuna hakikisha kuwa zoezi hili na matokeo yake yanaleta mafanikio ya kudumu na kubadili maisha yao”Tuzo za mwanamakuka za mwaka huu zitafanyika sambamba na kusherehekea siku ya wanawake Dunia, Mwanamakuka family bonanza itafanyika tarehe 15 machi 2014 , siku ya Jumamosi katika viwanja vya Escape 1 Dar es Saalam kuanzia saa 4 asubuhi hadi saa 2 Usiku.

YANGA USO KWA USO NA AL-AHLY LEO.


Yanga ya Tanzania.
Al-Ahly ya Misri.
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Mabingwa barani Afrika, Young Africans, maarufu kama "Yanga" leo hii wanakabiliana na mabingwa watetezi wa kombe hilo, Al-Ahly ya Misri katika mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kuingia katika hatua ya raundi ya kwanza ya michuano hii, Yanga waliitupa nje timu ya Comorro, Komorozine kwa kuichabanga jumla ya magoli 12-2. Katika mchezo wa kwanza na Komorozine, uliofanyika jijini Dar es Saalm,Yanga iliitwisha mzigo wa magoli 7-0 na kuiadhibu tena nyumbani kwao Comorro mabao 5-2, hivyo kujikuta katika raudni ya kwanza ikipangiwa kukutana na al-Ahly.
Yanga imekuwa na msukumo mkubwa wa kupata ushindi baada ya mwenendo wake wa kufanya vizuri katika michezo ya kimataifa na ligi kuu ya nyumbani. Katika mapambano yaliyopita kati ya Yanga na Al-Ahly, daima timu hiyo ya Misri imekuwa ikiibuka mbabe kwa kuifunga na kuitoa Yanga katika mashindano kama hayo kwa zaidi ya miongo mitatu sasa, mthalani mwaka 2009, katika hatua kama hii Yanga ilichapwa na al-ahly mabao 4-0 na kutolewa nje.
Hata hivyo, safari hii, Yanga imeonekana kupania kusonga mbele katika michuano hiyo ya Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF, kwani imefanya maandalizi makubwa ikiwemo kupiga kambi ya wiki mbili nchini Uturuki, barani Ulaya na kuendelea kufanya vizuri katika ligi kuu ya nyumbani.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans Pluijn anajivunia kikosi chake na kutamba kwamba safari hii, al-Ahly hawatatoka salama katika Uwanja wa Taifa, akijigamba kwamba atawafunga kwani anazifahamu vizuri mbinu za timu hiyo.

Mechi nyingine zitakazochezwa leo za mabingwa wa kombe la Afrika ni Gor Mahia ya Kenya watakuwa wenyeji wa EST ya Tunisia, Kampala City Council ya Uganda itasafiri kwenda Zambia kumenyana na Nkana Red Devil.

DIAMOND, MADEE, CHEGE NA TEMBA WAFANYA KWELI TAMASHA LA COCA COLA ZOO.

Diamond Platnum him self  akionyesha style yake ya ngololo inavyochezwa mbele ya umati wa mashabiki waliofurika vyakutosha kwenye uwanja wa Furahisha Kirumba jijini Mwanza ambapo msanii huyo alipiga bonge la show.
Platnum kama balozi wa coca cola nae ndani  Burudani mwanzo mwisho.
Madee katika stage nani!! kamwaga soda yangu..........
Madee na mistari yake akiburudisha mashabiki waliofurika kwa wingi uwanja wa Furahisha Kirumba jijini Mwanza.
Madee.
 

Katika stage sasa ni zamu ya Chege Chigunda na Mheshimiwa Temba kukisanukisha kwenye stege la viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
Wanaume kazini.
Watu nyomi si mchezo siunajua show ya bure...
Chege na Temba kama kawaida yao.
Chege chigunda kwenye stage.
Mh Temba.
Maurice Njoweka ambaye ni Meneja wa Bidhaa ya Cocacola akizungumza na waandishi wa habari juu ya tamasha hilo kubwa lililonuia kutoa burudani kwa mashabiki wa Mwanza kama sehemu ya shukurani kwao kwa kuziamini bidhaa za Coca cola na kuzitumia.
Enjoy your drink.
Palikuwa hapatoshi.

CCM WAZINDUA KAMPENI KALENGA.


Kwenye uzinduzi wa kampeni jimbo la Kalenga jana CCM ulio fanyika  Ifunda.

Msanii Dokii akifanya yake katika kampeni  
Kushoto gari la m4c  na kulia gari lililobeba wanachama wa chama cha mapinduzi wakielekea kwenye mkutano wao.

BUS LA BUNDA EXPRESS LAPATA AJALI SINGIDA KWA KUGONGANA NA TRENI.

bunda2

Hii ni Taarifa kutoka Mkoani Singida ambapo Habari zilizotoka zinahusisha ajali iliyohusisha Basi la Bunda Bus lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Mwanza asubuhi ya February 28 limegongana na Treni Eneo la Manyoni mkoani Singida.
Chanzo cha ajali hiyo hakijajulikana ingawa inawezekana ni sababu ya Bus hilo kuingia njia ya treni,mpaka sasa idadi kamili ya majeruhi na waliopoteza maisha bado haijatangazwa,millardayo.com bado inafatilia chanzo cha ajali hii.  


                                              Hili ni treni lilo gongana na bus

CLOUDS YAPATA KIBALI CHA KURUSHA MATANGAZO NCHI NZIMA.

1779281_684969414879813_999306451_n
Leo hii tarehe 28/2/2014 Clouds TV  imepata kibali cha kurusha matangazo yake Tanzania nzima.
Clouds TV imekabidhiwa kibali hicho na Tanzania communications regulatory authority (TCRA).
General director wa TCRA Prof John Nkoma amemkabidhi director of production and programs wa Clouds media group Mr Ruge Mutahaba kibali cha Clouds TV kurusha matangazo yake nchi nzima kama free to air.
1619427_684969471546474_711060175_n 
Cetficate waliyopewa clouds tv

Dr.MAGUFULIAKAGUA MRADI WA MABASI YAENDAYO KASI JIJINI DAR ES SAALAM

Dr.John Magufuli kwa mara nyingine amefanya ukaguzi wa maendeleo ya mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (BRT) Jijini Dar es Salaam akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Katibu Mkuu- Ujenzi, Katibu Mkuu -TAMISEMI, Kamati ya Ulinzi na Usalaam ya Mkoa wa Dsm, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara-TANROADS,Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usafiri wa Haraka -DART, Meneja wa Ujenzi wa Mradi pamoja na wadau mbalimabli wa mradi wakiwemo wananchi.
Dr.Magufuli amehoji kiasi kikubwa cha mzigo kupitia barabarani badala ya reli, ambapo asilimia 98.7 ya mizigo inayosafirishwa mikoani inapita barabarani hasa kutoka DSM kwenda Tunduma sehemu inayofikika kwa reli.
Ili kupunguza msongamano, amesema miradi saba (7) iliyopo jijini Dsm ipo mbioni kusainiwa wakatai wowote, hata hivyo amesisitiza wananchi wa kada zote kufuata sheria zilizowekwa ikiwa ni pamoja na kupisha hifadhi za barabara, sheria za barabara n.k.
Aidha, Dr.Magufuli amegusia na kusisitiza kuanza kwa ujenzi wa barabara ya kiwango cha EXPRESSWAY inayotoka Dar - es Salaam hadi Chalinze yenye urefu wa kilomita 100, barabara hii itakuwa ya njia sita hadi nane kila upande. Makampuni yapatayo kumi na tisa yameonyesha nia ya kuwekeza kwa kuingia ubia na Serikali ya Tanzania kupitia utaratibu wa Public Private Partnership (PPP). Kwa kuzingatia kiwango cha EXPRESSWAY mradi huo utahitaji eneo kubwa la ujenzi (Construction Corridor) . Dr.Magufuli amewakumbusha wananchi waliovamia hifadhi ya barabara (Road Reserve) kupisha mara moja ili kuepuka usumbufu kipindi mradi utakapoanza, pia amewashauri wananchi wasipotoshwe na baadhi ya watu kuhusu hifadhi ya barabara ya Morogoro kwa kuwa upana wa barabara hii unajulikana kuwa ni tofauti na barabara zingine nchini, yeyote atayekaidi kwa kutumia kesi batili atafikishwa mahakamini.
Picha za matukio ya msafara wa waziri wa Ujenzi Dr.Magufuli;







Ndani ya Basi liendalo Haraka




Wakala wa Usafiri wa Haraka -DART


Kazini

Akipata Maelezo ya Mradi


Akipata Maelezo ya Mradi kutoka kwa Meneja wa Mradi-TNROADS